AVEVA NA KABURU WAENDELEA KUSOTA RUMANDE KESI YASOGEZWA MBELE

Kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili Rais wa Simba, Evance Aveva na makamu wake Geofrey Nyange 'kaburu' imesomwa leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Watuhumiwa hao wawili wamerejeshwa rumande kutokana na upelelezi wa kesi yao kutokamilika na sasa kesi hiyo itasomwa tena Agosti 7 mwaka huu.


Mara ya mwisho kesi hiyo iliposomwa, Kaburu hakuhudhuria kutokana na matatizo ya kiafya, lakini leo alikuwepo mahakamani.

No comments

Powered by Blogger.