STARS HII UNAACHAJE KUIPENDA SASA! YAIVUA UBINGWA AFRIKA KUSINI
Timu ya Taifa ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya vyama vya soka kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya kuwafunga wenyeji Afrika Kusini kwa bao 1-0.
Alikua ni Mshambuliaji Wa zamani wa Simba na Stand United Elias Maguli ambaye anacheza soka la kulipwa hivi sasa huko Uarabuni aliyeipatia Stars bao pekee dakika ya 18 baada ya kazi nzuri ya Mzamiru Yasin.
Bao hilo liliwachanganya zaidi Afrika Kusini ambao walikua ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo kwani licha ya juhudi kubwa za kulishambulia lango la Stars mipira iliishia mikononi mwa Kipa Aishi Manula au kutoka nje kwa dakika zote 90.
Kwa matokeo hayo sasa Taifa Stars wanatinga hatua ya nusu fainali wakati wenyeji Afrika Kusini ndo basi tena wameaga michuano hiyo.
Mshambuliaji Elias Maguli licha ya kufunga bao hilo lakini pia ndiye aliyekua mchezaji bora wa mchezo huo akipata tuzo na dola 50 toka kwa wadhamini Castle Lager.
HONGERA STARS MAPAMBANO YANAENDELEA
No comments