SARAKASI UCHAGUZI TFF KISA WANAOTAKA KUMRUDISHA MALINZI.


Katika hali isiyotarajiwa na wengi uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF umeingia katika hali ya sintofahamu baada ya mwenyekiti wa Uchaguzi huo REVOCATUS KUULI kusimamisha mchakato wa uchaguzi huo.

Akiongea na waandishi wa habari Kuuli amesema
"Siwezi Kuendelea Na machakato Usio kuwa Na haki watu wanawakata watu Bila sababu Za Msingi! Uonevu Huo Nimeshindwa Kuuvumilia, nimeona kwakua Nina mamlaka yakusitisha Mchakato Basi Nimwandikia Katibu mkuu.. Barua Na yeye Akakaa Na Sekretariet, Wamekubali Ombi hilo. Hivyo Kuanzia Sasa mchakato Wa uchaguzi umesitishwa Mpaka pale Utakapo tangazwa Tena."

Wapo baadhi ya wajumbe waliokua wakilazimisha kusailiwa Jamal Malinzi wakati hakuwepo ukumbini kama kanuni zinavyotaka  Kama ingekua ni rahisi hivyo basi kusingekua na haja mtu akatoka Kagera kuja kufanya usaili Dar angeandika tu barua" alisema Kuuli.

Jana ilikua siki ya mwisho ya usaili wa wagombea katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho hilo uliopangwa kufanyika mwezi ujao mjini Dodoma.

No comments

Powered by Blogger.