GERMANY YASHINDA KOMBE LA MABARA KWA MARA YA KWANZA


Mabingwa wa Dunia Ujerumani wameibuka washindi wa kombe la mabara wakishinda bao 1-0 dhidi ya Chile ambao ni mabingwa wa Amerika Kusini.

Ujerumani ambayo imechezesha vijana wengi katika michuano hiyo ilifanikiwa kupata bao lao pekee dakika ya 20 ya mchezo likifungwa na Lars Stind.

Huu ni ubingwa wa kwanza kwa Ujerumani katika historia ya kombe la mabara ikiwa timu ya pili baada ya Ufaransa kushinda ubingwa huu wakiwa ni mabingwa wa kombe la dunia.

Michuano hiyo ilikua ni maandalizi ya michuano ya kombe la dunia mwakani nchini Russia.

Kipa wa Chile Claudio Bravo ameibuka kipa bora wa michuano hiyo wakati Julian Draxler akiibuka kama mchezaji bora wa michuano hiyo.

No comments

Powered by Blogger.