MONACO YAENDELEA KUMNG'ANG'A MBAPPE


Klabu ya Monaco imesema hakuna ofa yoyote iliyokubaliwa kwa ajili ya kumuuza nyota wao ghali zaidi kwa sasa Kylian Mbappe

Gazeti la Macca limeripoti kwamba Real Madrid wamepeleka ofa ya £160 Milioni kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 18 tu ambaye alifunga mabao 26 katika ligi kuu ya Ufaransa msimu uliopita na kuisaidia Monaco kutwaa ubingwa.

Taarifa hiyo ya gazeti la Macca la Hispania imewashtua wengi kutokana na kiasi kikubwa sana cha pesa kwa ajili ya kijana huyo ukizingatia umri wake mdogo.

Rekodi ya usajili duniani kwa sasa inashikiliwa na uhamisho wa kiungo wa mfaransa Paul Pogba ambaye alisajiliwa na Manchester United kutoka Juventus kwa ada inayofikia £93 milioni.

No comments

Powered by Blogger.