RAYON SPORTS KUNOGESHA SIMBA DAY

Imefahamika kwamba klabu ya Rayon Sports ya Rwanda ndiyo itakayoshiriki katika kilele cha sherehe za Simba Day mnamo Agosti 8 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Simba Day ni tamasha ambalo hufanyika kila mwaka hapa nchini likitumiwa na klabu ya Simba kutambulisha wachezaji wake pamoja na jezi watakazozitumia kwa msimu husika.

Sambamba na hilo, Simba imekua na kawaida ya kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki katika siku hiyo ambapo timu mbalimbali zimewahi kualikwa na sasa ni zamu ya klabu hiyo kongwe nchini Rwanda.

Bado haijafahamika ni lini hasa Rayon watawasili nchini, lakini taarifa zinasema tayari wameukubali mwaliko huo na watakuwepo kuzijaribu bunduki mpya za Simba kwa ajili ya msimu ujao.

No comments

Powered by Blogger.