LUKAKU AFUNGUA KITABU CHA MABAO MAN UNITED IKIIADHIBU REAL SALT LAKE
Mshambuliaji mpya wa manchester United Romelu Lukaku amefanikiwa kufungua ukurasa mpya kwenye maisha yake akifunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na Manchester United akitokea Everton.
Lukaku alifunga moja kati ya mabao mawili katika ushindi wa bao 2-1 walioupata Manchester united dhidi ya Real Salt Lake inayoshiriki ligi kuu ya Marekani MLS.
Henrik Mkytaryan aliisawazishia United bao la kwanza walilotanguliwa kufungwa na baadaye Mkhtaryan akamtengenezea Lukaku aliyewapiga chenga mabeki na kipa wa Real Salt Lake hatimaye kuuweka mpira wavuni.
Man United inaendelea na maandalizi yake kwaajili ya msimu ujao na kesho kutwa itacheza dhidi ya Manchester City kwenye michuano ya International Champions Cup ambayo inashirikisha pia Real Madrid na Barcelona.
No comments