STARS KUTUA RWANDA KESHO.
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inataraji kuondoka jijini Mwanza kesho asubuhi kuelekea nchini Rwanda tayari kwa mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa michuano ya Afrika wa wachezaji wanaocheza soka la ndani, CHAN
Stars inataraji kuondoka Mwanza kesho majira ya saa nne asubuhi lakini italazimika kurudi Dar es Salaam katika uwanja wa kimataifa JK Nyerere ili kuunganisha safari na ndege ya kuelekea Rwanda.
Stars inataraji kutua JKNIA majira ya saa sita mchana na kuondoka mnamo saa nane kuelekea Rwanda tayari kwa mchezo huo utakaopigwa July 22.
Katika mchezo wa kwanza, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 hali inayoilazimu Stars kushinda au kutoa sare ya kuanzia mabao mawili katika mchezo wa marudiano.

No comments