JAMES MSUVA AFUZU MAJARIBIO MBAO FC.

James Msuva ambaye ni mdogo wake na nyota wa Yanga na Taifa Stars Saimon Msuva, ameibukia katika mazoezi ya Mbao FC ya Mwanza ambako amefanya majaribio na kufuzu.

James ambaye kwa nyakati tofauti amewahi kuvichezea vikosi vya vijana vya Simba na Yanga aliichezea JKT katika msimu uliopita wa ligi kuu.

Kocha wa Mbao Etienne Ndayiragije amesema amewajaribu wachezaji wengi kwa ajili ya kujenga kikosi chake ambacho kimeondokewa na nyota kadhaa.


Ndayiragije amesema wapo waliofuzu majaribio hayo akiwemo James hivyo kinachofuata ni viongozi kusaini naye mkataba ili akitumikie kikosi hicho msimu ujao.

No comments

Powered by Blogger.