CONTE ABORESHEWA MAISHA CHELSEA
Mabingwa
wa ligi kuu ya Uingereza, Chelsea, wamempa mkataba mpya wa miaka miwili kocha
wao aliyewapa ubingwa Antonio Conte.
Mkataba huu mpya ni sawa na maboresho ya ule wa
awali wa miaka mitatu ambao Conte alisaini Julai mwaka jana ukimweka klabuni
hapo hadi mwaka 2019.
Mkataba huu mpya unakwenda kuboresha maslahi ya
kocha huyo ambaye anajiandaa na safari ya kuelekea barani Asia kwa ajili ya
michezo ya kirafiki ambapo Chelsea watacheza dhidi ya Arsenal na Bayern Munich.
Akiuzungumzia mkataba huo, Conte amesema
anafuraha kusaini mkataba mpya baada ya mafanikio makubwa katika mwaka wake wa
kwanza huku na kwamba wanajiandaa kwa ajili ya kusalia kileleni.

No comments