KIPA BORA COSAFA ATUA SIMBA.
Simba bado wapo 'busy' wakikisuka kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao. Wameendelea kutumia fedha kusajili nyota wenye uwezo mkubwa kwa ajili ya kujiimarisha na taarifa mpya ni kwamba wamemnasa kipa wa Mtibwa na Taifa Stars, Said Mohamed maarufu kama Nduda.
Nduda ni golikipa mzoefu hapa nchini na aliwahi
kuzidakia Majimaji na Yanga kabla ya kuibukia Mtibwa.
Kipa huyo ambaye hivi karibuni alitwaa tuzo ya
golikipa bora akiwa na timu ya taifa, Taifa Stars katika michuano ya COSAFA
huko Afrika kusini, atakutana na upinzani mkali katika kikosi cha Simba kutoka
kwa makipa waliosajiliwa ambao ni Aishi Manula kutoka Azam FC na Emmanuel Mseja
kutoka Mbao FC.
Kwa sasa, Nduda yupo na kikosi cha timu ya taifa
ya Tanzania ambacho kinatua Kigali Rwanda leo kwa ajili ya mchezo wa marudiano
wa kuwania kufuzu michuano ya CHAN dhidi ya wenyeji Amavubi.

No comments