HISPANIA KAMA BONGO, RAIS WA SOKA ANASHIKILIWA.
Tunatambua
kwamba Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF, Jamal Malinzi anashikiliwa kwa
tuhuma mbalimbali zikihusu mambo ya fedha. Hali inayofanana na hiyo imetokea
huko Ulaya katika nchi ya Hispania.
Taasisi ya kuzuia rushwa ya nchi hiyo iitwayo
Unidad Central Operativa imemkamata na kumshikilia Rais wa shirikisho la soka
nchini humo Angel Maria Villar na mwanaye anayefahamika kwa jina la Gorka.
Wawili hao wameshikiliwa wakikabiliana na tuhuma
mbalimbali za rushwa na matumizi mabaya ya ofisi na taarifa zinasema
watafikishwa mahakamani muda wowote.

No comments