SANCHEZ HAUZWI. ASEMA WENGER.

Hatimaye kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameweka wazi msimamo wa klabu hiyo kumhusu mshambuliaji wake Alexis Sanchez ambaye amenukuliwa na vyombo vya habari akisema anataka kuondoka klabuni hapo.

Mkataba wa Sanchez na Arsenal umesaliwa na mwaka mmoja kumalizika, huku nyota huyo akinukuliwa na vyombo vya habari akisema anataka kucheza katika klabu bingwa Ulaya ambayo Arsenal haitoshiriki msimu ujao.

"Uamuzi umekwisha fikiwa na tutausimamia, Uamuzi ni kwamba hatutomuuza" alisema Wenger.

Wenger amesema anaamini Sanchez atakiongoza kikosi chake kurejea katika michuano hiyo ya Ulaya kupitia ligi kuu msimu ujao, huku akiikataa tafsiri ya kauli ya Sanchez kwamba anataka kuondoka.

"Siwezi kukaa hapa kuongelea vitu vilivyotafsiriwa, mimi nimeona mahojiano yote yale na kinachosemwa sicho kilichomaanishwa"

"Tunajiandaa na ligi sasa hivi, tumekua kwenye ligi ya mabingwa kwa miaka 20. Hiyo ni miaka 17 kabla Sanchez hajafika hapa na tumekua nae pale kwa miaka mitatu. Naamini atatusaidia kurejea pale" alisema Wenger.

Alexis Sanchez amekua akihusishwa na vilabu mbalimbali ikiwemo Manchester  City inayofundishwa na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola.

No comments

Powered by Blogger.