BOLASIE AMFUNIKA ROONEY MAPOKEZI YA EVERTON DAR ES SALAAM (+PICHA)
Everton FC kutoka katika Ligi kuu ya England tayari wako Dar es Salaam Tanzania kwa ajili ya mechi ya kirafiki Kesho alhamisi dhidi ya Mabingwa wa SportPesa Cup timu ya GorMahia kutoka Kenya.
Mchezo huo utapigwa majira ya saa 11 jioni kesho kwenye dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam na leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Everton ilipokelewa na waziri wa habari sanaa na Michezo Dr. Harisson Mwakyembe.
Yannick Bollasie Mchezaji wa kimataifa wa Congo DR ndiye aliyefunika kwenye mapokezi ya leo baada ya kupokelewa na Wacongo wengi waliojitokeza kumpokea tangu uwanja wa ndege mpaka Hotelini kwa ngoma na bendera
Tayari vyombo vya habari vya kimataifa vimesharipoti ujio wa Everton huku ikitarajiwa Tanzania kutangazwa zaidi baada ya mchezo wa kesho.
| wachezaji wakiongea na watoto shuleni Uhuru Mchanganyiko |
| Huyu ndiye Yannick Bolasie |
| Wamasai walikuwa kati ya waliowapokea wageni |
No comments