EVERTON "WAPASHA" TAIFA KUJIWEKA TAYARI KWA PAMBANO LA KESHO

Wakongwe wa Soka la England klabu ya Everton inaendelea na mazoezi ya jioni katika uwanja wa Taifa jijini ikiwa ni moja ya lengo lao la kuja hapa Tanzania.

Sambamba na kujiandaa na mechi ya kesho dhidi ya mabingwa wa SportPesa Super Cup Klabu ya Gor Mahia toka nchini Kenya,pia Everton wako nchini kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya England inayotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.

Evverton ilitua nchini asubuhi ya leo Jumatano Julai 12,2017 kwa Ndege maalumu toka jijini Liverpool Nchini England ikiwa na wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza akiwemo pia nahodha wa zamani wa Manchester United na England Wayne Rooney.

Kamera ya www.wapendasoka.com iko uwanja wa Taifa kushuhudia mazoezi ya wakali hao toka England na tutakua tunakupatia vidokezo muhimu kupitia kurasa zetu za facebook,Instagram na Twitter.

No comments

Powered by Blogger.