WATOTO MAPACHA WA RONALDO WAZALIWA DAKIKA CHACHE BAADA YA KUTOLEWA NA CHILE KOMBE LA MABARA

Yawezekana haukuwa usiku mzuri sana uwanjani kwa upande wa Nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo lakini umekua usiku mzuri zaidi kwake nje ya uwanja baada ya kupata watoto wawili mapacha wa kiume muda mchache baada ya mechi ya nusu fainali kombe la mabara jana usiku.
Ronaldo confirmed the news just hours after Portugal's exit from the Confederations Cup
Ronaldo akiwa na Ureno walikubali kuondolewa katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kufungwa kwa penati 3-0 na mabingwa wa Amerika Kusini Chile.


Mara tu baada ya mchezo huo Ronaldo alitumia akaunti yake ya Facebook kutoa habari za watoto hao mapacha waliozaliwa nchini Ureno baada ya pandikizi ya kuwapata kwa kuunganisha mbegu zake kwa Mwanamke aliyebeba ujauzito na hatimaye wakapatikana.

Tayari Ronaldo ana mtoto mmoja mwenye miaka 7 Cristiano Ronaldo jr na huenda familia yake ikaongezeka zaidi ndani ya miezi mitano ijayo baada ya Mchumba wake wa sasa Georgina Rodríguez kuonekana ana ujauzito wa miezi mitano.

Ronaldo ameruhusiwa kurejea nyumbani kuwa karibu na familia yake baada ya mechi ya jana huku Ureno ikikabiliwa na mechi ya mwisho kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Mexico au Ujerumani wanaocheza leo.

No comments

Powered by Blogger.