WANASOKA WA ZAMANI WAJITOSA KUWANIA UONGOZI TFF
Mshambuliaji wa zamani wa Simba Mtemi Ramadhani na Kiungo wa zamani wa Yanga Ali Mayai Tembele wamechukua fomu za kuwania nafasi tofauti za uongozi wa shirikisho la soka nchini TFF.
Ally Mayay yeye amechukua fomu ya kuwania Urais wa shirikisho hilo ambapo atachuana na wagombea ambao mpaka sasa ni Rais wa sasa Jamal Malinzi, Athumani Nyamlani, Iman Madega na Wallace Karia
Mtemi yeye atawania nafasi ya makamu wa Rais wa Shirikisho hilo akichuana na Geofrey Nyange 'Kaburu',
Michael Wambura na Mulamu Ng'ambi. mpaka sasa.

No comments