UCHAGUZI TFF: 62 WAPIGANA VIKUMBO KUWANIA NAFASI ZILIZOTANGAZWA


Juni 16, 2017 kipenga cha uchaguzi wa Shirikisho la Mpira Wa Miguu Tanzania (TFF) kilipulizwa. Kwa Muda wote huo wanamichezo mbalimbali wamejitokea kugombea nafasi mbalimbali kama zilivyotangazwa.


Katika uchaguzi huo, nafasi zinazogombewa ni pamoja na Rais wa Shirikisho, Makamu Wa Rais na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kutoka katika kanda 13.

Gharama za kuchukua fomu ni
a) Rais Tsh. 500,000/=
b) Makamu wa Raisi Tsh. 300,000/=
c) Mjumbe wa Kamati Ya Utendaji Tsh. 200,000/=

Kesho Jumanne, 20/6/2017 saa kumi (10:00) Jioni ndiye inategemewa kuwa mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu katika ofisi za TFF, Karume Dar es Salaam, Uchaguzi Unatarajia kufanyika 12/08/2017, huko katika makao makuu ya nchi Dodoma, Tanzania

Sifa za Mgombea
  1. Awe raia wa Tanzania.
  2. Awe na kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne (Cheti cha   Elimu ya Sekondari).
  3. Awe na uzoefu wa uendeshaji Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano.
  4. Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na asiwe amewahi kuhukumiwa kifungo kisicho na mbadala wa faini.
  5. Awe na umri angalau miaka 25.
  6. Awe amewahi kuwa ama Mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi. Au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu angalau katika ngazi ya Mkoa au ngazi ya daraja la kwanza.
  7. Awe muadilifu na muaminifu mwenye uwezo wa utendaji katika utekelezaji na utimizaji wa majukumu na malengo ya TFF.
  8. anayegombea nafasi ya Rais au makamu wa Rais awe na kiwango cha elimu kisichopungua shahada moja, mwenye utu na uwezo wa kuiwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.

Walichukua fomu mpaka sasa ni pamoja na Jamal Malinzi, Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Athumani Nyamlani, wengine waliochukua fomu hizo ni Fredrick Mwakalebela na Ally Mayay wakati waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais wako Mulamu Nghambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani na Robert Selasela.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:

Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita;
  1. Soloum Chama
  2. Kaliro Samson
  3. Samwel Daniel
  4. Leopold Mukebezi
  5. Abdallah Mussa

Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;
  1. Vedastus Lufano
  2. Ephraim Majinge

Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu;
  1. Benista Rugora
  2. Mbasha Matutu
  3. Stanslaus Nyongo

Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara;
  1. Omari Walii
  2. Sarah Chao
  3. Peter Temu

Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora;
  1. John Kadutu
  2. Issa Bukuku
  3. Abubakar Zebo

Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa;
  1. Kenneth Pesambili
  2. Baraka Mazengo

Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya na Iringa;
  1. Elias Mwanjala
  2. Cyprian Kuyava
  3. Erick Ambakisye

Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma;
  1. James Mhagama
  2. Golden Sanga
  3. Vicent Majili

Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;
  1. Athuman Kambi
  2. Dunstan Mkundi

Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida; 
  1. Hussein Mwamba
  2. Mohamed Aden
  3. Musa Sima
  4. Stewart Masima 
  5. Ally Suru
Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro;
  1. Charles Mwakambaya
  2. Gabriel Makwawe
  3. Francis Ndulane 

Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga
  1. Khalid Mohamed
  2. Goodluck Moshi

Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam
  1. Emmanuel Ashery
  2. Ayoub Nyenzi
  3. Saleh Alawi
  4. Shaffih Dauda
  5. Thabit Kandoro
  6. Abdul Sauko
  7. Peter Mhinzi
  8. Ally Kamtande
  9. Said Tully
  10. Mussa Kisoky
  11. Lameck Nyambaya
  12. Ramadhani Nassib
  13. Aziz Khalfan


No comments

Powered by Blogger.