MOTO WA KOMBE LA MABARA WAANZA URUSI, AFRIKA HOI

Michuano ya kombe la mabara inaendelea nchini Urusi, tumeshuhudia michezo miwili ikipigwa jana katika michuano hiyo
Mchezo wa mapema ulikuwa ni kati ya Ureno na Mexico na timu hizo zote kutoshana nguvu kwa sare ya mabao 2-2 Magoli ya Ureno yalifungwa na Ricardo Quaresma na Soares, huku magoli ya Mexico yakifungwa na mshambulia wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez Chicharito na Moreno.

Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya mabingwa wa Afrika Cameroon na mabingwa wa Amerika ya kusini Chile huku tukishuhudia Cameroon wakilala kwa mabao 2-0 Magoli ya Chile yakifungwa na Arturo Vidal na Eduardo Vargas.

No comments

Powered by Blogger.