UCHAGUZI T.F.F: WAKATI WAMBURA AKIMKIMBIA MALINZI,MADEGA AJITOSA KUPAMBANA NAE
Madega amechukua fomu hizo leo asubuhi muda mfupi baada ya Rais wa sasa wa shirikisho hilo Jamal Malinzi naye kuchukua fomu kwa ajili ya kutetea nafasi yake.
Mpaka sasa nafasi ya urais wa TFF imepata wagombea wawili ambao ni Malinzi na Madega, huku zoezi la uchukuaji fomu likiendelea.
Wakati viongozi hao wa siku nyingi katika soka Tanzania wakiutaka urais, nguli mwingine Michael Richard Wambura ambaye aliwahi kuwa katibu mkuu wa kilichokua chama cha soka Tanzania FAT yeye ameamua kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti.
Wambura ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoani Mara amechukua fomu leo kwa ajili ya nafasi hiyo.

Michael Wambura mtu mpiganaji sana
ReplyDelete