USAJILI WA MBARAKA YUSUPH KUIGHARIMU AZAM FC, KAGERA WADAI MILIONI 150
Timu ya Kagera Sugar imeibuka na kudai ina mkataba na mshambuliaji Mbaraka Yusuf Abeid ambaye ametimkia Azam kama mchezaji huru.
Kwa mujibu wa kiongozi wa klabu hiyo, Mohamed Hussein, amesema Mkataba walionao na mshambuliaji huyo wa Taifa Stars umesaliwa na mwaka mmoja na wao tayari wamepeleka malalamiko TFF.
Pamoja na malalamiko yao, Kagera Sugar wamedai watamruhusu nyota huyo kujiunga na Azam lakini wanahitaji walipwe Shilingi milioni 150 kama ada ya uhamisho.
Mbaraka Yusuf alijiunga na Azam hivi karibuni akitajwa kulamba dau la shilingi milioni 40 kama mchezaji huru.

No comments