STARS YAONDOKA NA MATUMAINI TELE MICHUANO YA COSAFA

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kitasafiri jioni ya leo kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya michuano ya Baraza la Michezo Kusini mwa Afrika (Cosafa) itakayoanza Juni 24.

Kocha mkuu wa timu hiyo Salum Mayanga amewaambia Waandishi wa Habari kuwa kikosi chake kipo timamu kwa michuano hiyo sababu wachezaji wake wana morali ya hali ya juu.

"Kikosi kipo tayari kwa michuano hiyo ambapo wachezaji wako vizuri isipokuwa mshambuliaji Shaban Idd ambaye aliumia na ripoti za daktari inasema atakuwa fiti baada ya siku tatu," alisema Mayanga.

Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo Himid Mao amewataka Watanzania kuwapa sapoti ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano hiyo na kukiri kuwa hawata waangusha.

"Sisi wachezaji tumejipanga kufanya vizuri, tutafuata maelekezo ya mwalimu na tunawaomba Watanzania watupe sapoti," alisema Himid.

Tanzania timu mwalika kwenye michuano hiyo kutokana na kutokuwa mwanachama wa Cosafa.

No comments

Powered by Blogger.