MEXICO NA URENO WATAMBA KOMBE LA MABARA, NEW ZEALAND WAAGA.

Michuano ya Kombe la Mabara imeendelea tena jana kwa mchezo wa mapema uliowakutanisha Mabingwa wa ulaya Portugal na wenyeji wa michuano hiyo Urusi .

Ureno waliibuka vinara kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Urusi huku
Goli pekee la Ureno likifungwa na mshambuliaji Cristiano Ronaldo katika dakika ya 8 ya mchezo kwa kichwa maridadi.

Mchezo wa pili ulikuwa kati ya Mexico na New Zealand, Mexico wakitoka nyuma walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 na hivo Mexico kuongoza Kundi A wakiwa na pointi 4 huku wakifuatiwa na Ureno wenye point 4 wakitofautiana kwa Magoli.

New Zealanda walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wake Chris Wood na Mexico wakasawazisha kupitia kwa Raul Jimenez huku bao la ushindi likifungwa na Oribe Peralta.
New Zealand inakuwa timu ya kwanza kuaga michuano hiyo.

No comments

Powered by Blogger.