OKWI KUTUA JUMAMOSI NA KUSAINI MIWILI SIMBA
Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Okwi kurejea Simba kutokana na kuitumikia timu hiyo kwa mapenzi mapenzi makubwa na mafanikio pia.
Usajili huo unakuja siku mbili baada ya taarifa kutoka kuwa Simba imekamilisha usajili wa kiungo fundi kutoka Yanga Haruna Niyonzima.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hanspope amewaambia Waandishi wa Habari kuwa mchezaji huyo atatua nchini Jumamosi na kusaini mkataba wa miaka miwili.
"Nilikuwa Uganda wiki iliyopita nikafanya mazungumzo na Okwi tukakubaliana kila kitu na keshokutwa Jumamosi atatua nchini na kusaini mkataba wa miaka miwili."

No comments