RONALDO AIPELEKA URENO NUSU FAINALI KOMBE LA MABARA
Mshambuliaji na nahodha wa timu ya Taifa ya Ureno ambaye pia ni mchezaji bora wa dunia Cristiano RONALDO Jana usiku aliiongoza Ureno kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mabara inayoendelea nchini Urusi.
Ronaldo alifunga bao moja katika ushindi wa bao 4-0 walioupata dhidi ya New Zealand mchezo wa kundi A ambapo Bernardo Silva, Andre Silva na Luis Nani pia walifunga.
Katika mechi nyingine ya kundi Hilo la A wenyeji Urusi walitupwa nje ya michuano hiyo baada ya kufungwa bao 2-1 na Mexico.
Leo zitapigwa mechi mbili za mwisho Leo katika hatua ya makundi baina ya Ujerumani na Cameroon wakati Chile wao watacheza dhidi ya Australia ambapo timu mbili zitatinga hatua ya nusu fainali.

No comments