NDOTO YA FARID MUSSA KUCHEZA LALIGA YAYEYUKA, TENERIFE YASHINDWA KUPANDA DARAJA
Ndoto ya Watanzania kumshuhudia mchezaji wa kitanzania akicheza katika moja ya ligi bora duniani yani ligi kuu ya Spain La liga imefutika baada ya Tenerife kushindwa kupanda daraja.
Tenerife Ndiyo Timu ambayo Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Farid MUSSA anaichezea akitokea Azam FC na usiku wa Jana walipoteza mechi muhimu wakifungwa bao 3-1 na Getafe.
Tenerife ilihitaji sare tu iweze kupanda daraja baada ya ushindi wake wa bao 1-0 katika mechi ya awali hivyo kupoteza kwa jumla ya Golgi 3-2.

No comments