POGBA FOUNDATION YAZINDULIWA KWA USHINDI MNONO


Mchezaji ghali zaidi kwasasa duniani Paul POGBA amezindua Foundation Yake ambayo itahusika na utoaji wa misaada kama ilivyo ada ya Foundation nyingi zinazozinduliwa na Wachezaji.

POGBA FOUNDATION ilizinduliwa nchini Colombia katika mechi dhidi ya Cuadrado Foundation ambayo ilianzishwa na Mchezaji wa kimataifa wa Colombia anayeichezea Juventus kwa mkopo akitokea Chelsea Juan Cuadrado.

Paul POGBA aliungana na kaka zake Mathias na Florentin katika mechi hiyo ambayo mapato Yake yatatumika kukuza vipaji nchini Colombia wakicheza dhidi ya Kikosi cha Cuadrado Foundation.

Mchezo huo ulimalizika kwa POGBA FOUNDATION kuibuka na ushindi wa bao 6-3 huku Mathias Pogba akifunga bao 2 peke Yake katika mechi ambayo David  Ospina na Carlos Bacca nao waliichezea Cuadrado Foundation.

No comments

Powered by Blogger.