ARSENAL "YAIBIPU" MAN UNITED, YATENGA FEDHA KUMNASA ANTHONY MARTIAL
Klabu ya Arsenal imetenga kiasi cha paundi milioni 40 kumnasa nyota wa kimataifa Wa Ufaransa anayeichezea Manchester United Anthony Martial iwapo watamkosa mshambuliaji Wa Monaco Kylian Mbappe ambaye inaonekana anaweza kwenda Real Madrid.
Mtihani mkubwa kwa kocha wa Arsenal ni Jose Mourinho ambaye haijajulikana kama atakubali kumuuza mchezaji huyo kwa wapinzani wao.
Martial ni mmoja wa wachezaji ambao wanaonekana kutokua na furaha katika Kikosi cha United tangu alipowasili kocha Jose Mourinho na ameonekana sio chaguo la kwanza la kocha huyo huku kukiwa na taarifa nyingi za United kutaka kuwasajili mawinga hivyo kutishia nafasi ya Martial kikosini.

No comments