SIMBA AKILI NYINGI: NAFASI YA AJIBU KUZIBWA NA OKWI, ATUA NCHINI KABURU ATOA NENO


MSHAMBULIAJI Emmanuel Okwi amewasili nchini usiku wa kuamkia leo akitokea nchini Uganda kwa ajili ya kusaini mkataba na mabingwa wa kombe la FA wekundu wa Msimbazi Simba.

Okwi aliwasili kwenye uwanja wa JK Nyerere saa Nne na nusu Usiku na kupokelewa na Makamu wa Rais wa klabu ya Simba Gofrey Nyange Kaburu na kuondoka nae kwenye gari ndogo.

Aidha Kaburu alipotafutwa na www.wapendasoka.com kuhusu ujio wa mchezaji huyo kipenzi cha mashabiki wa Simba kama Okwi ameshasaini kuichezea Simba au hapana amesema "Usajili wa Okwi unakaribia kukamilika na makubaliano ya awali yalishafanyika wiki kadhaa zilizopita ambapo yalibaki mambo madogo kabla ya kusaini mkataba kamili siku ya kesho," alisema Kaburu.

Okwi amekuwa kipenzi cha Mashabiki wa Simba kabla ya kuondoka na urejeo wake kwa Wekundu hao umepokelewa kwa mikono miwili hasa ukizingatia tayari Ibrahim Ajibu ameshaondoka klabuni hapo. 

Simba imeonekana kufanya usajili wa nguvu msimu  huu ili kujiweka tayari na ligi kuu  msimu ujao na michuano ya kimataifa. 

No comments

Powered by Blogger.