KOMBE LA MABARA: UJERUMANI YATINGA FAINALI KIBABE

Mabingwa wa Kombe la Dunia timu ya taifa ya Ujerumani jana usiku walitinga katika fainali ya michuano ya kombe la mabara baada ya kuikandamiza Mexico bao 4-1.

Mchezo huo wa nusu fainali ya pili ulishuhudia Ujerumani ambayo imepeleka vijana wengi kwenye michuano hiyo ikionyesha kandanda safi na kufungua akaunti ya magoli kupitia kwa Leon Goretzka jina geni kabisa katika soka duniani aliyefunga mabao mawili dakika ya 6 na dakika ya 8 baada ya mchezo kuanza.

Timo Werner na Amin Younes walifunga mabao mengine mawili kwa Ujerumani huku goli pekee la Mexico likifungwa na Marco Fabian.

Kwa matokeo hayo Ujerumani sasa watakutana na Chile katika mchezo wa fainali siku ya Jumapili huku Mexico wakivaana na Ureno kutafuta mshindi wa tatu siku ya Jumamosi.

No comments

Powered by Blogger.