HAWA NDIYO WATOTO MAPACHA WA CRISTIANO RONALDO
Mchezaji bora wa Dunia Cristiano Ronaldo Juzi alibarikiwa kupata watoto wawili mapacha wa kike na wa kiume na kupitia ukurasa wake wa facebook Ronaldo aliweka Picha akiwa na watoto wake hao wawili.
"Nina Furaha kuwashika wanangu wawili ambao ni upendo mpya katika maisha yangu" Aliandika Ronaldo maneno ambayo yaliambatana na picha hiyo hapo juu.
Ronaldo mwenye miaka 32 hivi sasa amewaita wanae majina ya Mateo na Eva akiwa sasa na watoto watatu baada ya Cristiano Ronaldo Jr mwenye miaka 7 hivi sasa.
No comments