URAIS WA MALINZI TFF NDO BASI TENA

Mbio za kutetea nafasi ya  Urais katika uchaguzi ujao kwa Rais wa Shirikisho la soka Tanzania bara Jamal Emily Malinzi zimefikia kikomo jana baada ya  Mhakama ya Kisutu kumrudisha Gerezani mpaka Julai 3.

Kauli aliyotoa Malinzi jana wakati akielekea Gereza la Keko kupitia kwa Mwanasheria wake zimeonyesha kabisa kwamba hana tena nafasi ya kutetea nafasi yake na kuwatakia mafanikio mema viongozi watakaochaguliwa.

"Mpira utaendelea kuwepo hata bila Malinzi na kwa uwezo wangu nilijitahidi kuhakikisha mpira unakua Tanzania. Nawaombea kila la heri viongozi watakaochaguliwa" Ilisema taarifa hiyo kutoka kwa Malinzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Soka mkoa wa Kagera.

Ukiacha taarifa hiyo Malinzi pamoja na Godfrey Nyange Kaburu ambao wote waliomba nafasi za kugombea katika uchaguzi ujao pia watakosa nafasi ya kushiriki katika zoezi muhimu la Usaili wa wagombea ambalo limeanza jana Katika ofisi za TFF Karume jijini Dar Es Salaam zoezi litakalodumu kwa siku 3 siku ambazo Malinzi na Kaburu watakua gerezani.

Uchaguzi mkuu wa TFF utafanyika Tarehe 12 Agosti Mjini Dodoma ambapo Shirikisho hilo sasa litapata viongozi wapya kabisa katika ngazi ya Rais na Makamu wake.

No comments

Powered by Blogger.