CONTE HANITAKI NAONDOKA CHELSEA ~ DIEGO COSTA


Mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Spain Diego Costa ameweka wazi kwamba ataihama klabu yake hiyo ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya England msimu ulioisha.

Costa anasema imemlazimu kufikiria wapi pa kucheza soka msimu ujao baada ya kocha wa Chelsea Antonio Conte kuweka wazi kwamba hamuhitaji tena katika kikosi chake kuanzia msimu ujao akimwachia ujumbe huo baada ya kumalizika kwa Ligi.

Costa mwenye miaka 28 hivi sasa alihuaishwa sana kutimkia nchini China mwezi Januari lakini hakufanikiwa na sasa inaonekana kabisa kuanza kutafuta timu ya kuichezea msimu ujao huku chaguo lake la kwanza lilikua ni kurejea katika klabu ya Atletico Madrid lakini dili hilo litashindikana kutokana na Atletico kukumbwa na adhabu ya kufungiwa kusajili kwa kipindi cha mwaka mzima.

Tayari Romelu Lukaku anatajwa kuziba nafasi ya Diego Costa utata ukibaki kuwa ni kiasi gani Chelsea na Everton watakubaliana na pesa za kumuuza Costa zitaisaidia Chelsea kumpata Lukaku ambaye klabu yake ya Everton inataka paundi milioni 100 kumruhusu.

AC Milan pekee ndiyo iliyotajwa kumwania Costa ili aweze kusajiliwa na tayari wawakilishi toka pande zote mbili wamekutana kukubaliana usajili wa mchezaji huyo ambaye ameshiriki katika upatikanaji wa mabao 68 ya Chelsea tangu ajiunge nayo idadi ambayo ni kubwa kuliko mchezaji yoyote katika kikosi cha Chelsea.


No comments

Powered by Blogger.