MONACO YAKARIBIA UBINGWA WA KWANZA UFARANSA BAADA YA MIAKA 17


Vinara wa ligi kuu ya Ufaransa Monaco wako mbioni kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Ufaransa kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1999/2000.

Monaco yenye falsafa ya mashambulizi zaidi msimu huu imeshafunga magoli 100 katika ligi kuu ya ufaransa pekee, huku zikisalia mechi mbili kumaliza kwa msimu huu na hapo jana waliweza kuibuka na ushindi wa bao 4-0 wakiifunga Lille.

Iwapo Monaco itashinda mechi yake ya Jumatano hii dhidi ya St. Ettienne au kupata sare tu basi itatawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Ligi kuu ya Ufaransa kwani itakua imefikisha pointi 90 kama itatoka sare ambazo hakuna timu itakayoweza kuzifikia.

Mfungaji bora wa timu hiyo mpaka sasa ni Radamel Falcao ambaye amefanikiwa kufunga mabao 20 mpaka sasa, huku kinda Kylian M'mbape akifuata nyuma kwa magoli 14.

No comments

Powered by Blogger.