DIRK KYUT AIPA FEYENOORD UBINGWA LIGI KUU YA UHOLANZI BAADA YA MIAKA 18


Magoli matatu ya mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Dirk Kyut yalitosha kuwapa ubingwa  klabu ya Feyenoord huko nchini Uholanzi, ikiifunga klabu ya Hercales bao 3-1.

Feyenoord iliyotakiwa kushinda mechi moja tu imenyakua ubingwa mbele ya vigogo wa nchini humo Ajax kwa tofauti ya pointi moja.

Hili ni taji la kwanza la ligi kwa Feyenoord baada ya miaka 18 tangu walipotwaa ubingwa kwa mara ya mwisho, mwaka 1998.

Kocha wa klabu iyo Giovanni Van Bronchorst amechezea na kupata mafanikio katika klabu za Arsenal mwaka 2000-2003, Barcelona 2004-2008.

Kabla hajaanza kuinoa Feyenoord alikua kocha msaidizi klabuni hapo kabla ya kupewa ukocha mkuu mwaka 2015, na msimu wake wa kwanza tu alifanikiwa kunyakua kombe la Mfalme la chama cha soka cha uholanzi KNVB mwaka 2016. Na mwaka 2017 ametwaa ubingwa wa Ligi.

No comments

Powered by Blogger.