LIGI YA MABINGWA : BAADA YA RONALDO KUFANYA YAKE WIKI ILIYOPITA LEO NI MARUDIO YA DERBY YA MADRID

Baada ya jana kushuhudia juventus ikiwa ni timu ya kwanza kutinga katika hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya leo utapigwa mchezo wa mwisho wa hatua ya nusu fainali baina ya wapinzani wakuu wa jiji la Madrid yani Mabingwa watetezi Real Madrid dhidi ya Makamu bingwa Atletico Madrid.

Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa katika dimba la Vicente Calderon nyumbani kwa Atletico Madrid ukiwa ni mchezo wa Mwisho baina ya timu hizo katika uwanja huo kwani kuanzia msimu ujao Atletico Madrid watahamia uwanja mwingine.

Katika Mechi ya wiki iliyopita Cristiano Ronaldo ambaye ndiye mchezaji bora wa dunia hivi sasa alifunga mabao yote matatu kwa Real Madrid katika ushindi wa bao 3-0 walioupata Real Madrid Nyumbani.

Matokeo ya wiki iliyopita yanaipa mlima mrefu wa kuupanda klabu ya Atletico Madrid kwani ili wapite watatakiwa kushinda bao 4-0 

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 4 kasorobo kwa saa za Afrika Mashariki.

No comments

Powered by Blogger.