BAADA YA KUSHUKA DARAJA, JKT YAJIPANGA KUREJEA LIGI KUU MWAKANI
Benchi la ufundi la maafande wa jeshi la kujenga Taifa JKT Ruvu ya Pwani umeahidi kuwa timu yao itapambana vyema kuhakikisha inarejea kuchezea ligi kuu msimu wa mwaka 2018/2019.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na www.wapendasoka.com kocha msaidizi wa klabu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la kujenga Taifa Azish Kondo alisema timu yao itahakikisha inapambana kumaliza mechi zao zilizobaki katika ligi kuu kupata ushindi na hakuna kudharau mechi yeyote hata kama matumaini ya kubaki katika ligi kuu yameshakufa na wako tayari kupambana kupata pointi dhidi ya Maji Maji FC na Ndanda FC.
Tayari JKT Ruvu imeshashuka daraja kutoka katika ligi kuu Tanzania bara na hii imekuja baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Toto Africans katika uwanja wa CCM Kirumba hivi karibuni.
Maafande hao katika msimamo wa ligi kuu wapo katika nafasi ya mwisho wakiwa na alama 23 baada ya michezo 28 wakiwa wameshinda mechi 3 na sare 10 huku wakifungwa michezo 15 huku wakiwa wamefungwa mabao 27 na kufunga mabao 15.

No comments