JUVENTUS YATANGULIA FAINALI MABINGWA ULAYA
Mabingwa wa Italia klabu ya Juventus jana usiku ilifanikiwa kutinga katika fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuitupa nje Monaco ya Ufaransa.
Ikicheza nyumbani Juventus ilifanikiwa kushinda kwa bao 2-1 ukiwa ni ushindi wa pili baada ya mechi ya awali ambapo Juventus waliibuka na Ushindi wa bao 2-0 hivyo kutinga fainali kwa ushindi wa jumla wa bao 4-1.
Mario Mandzukic na Dani Alves waliifungia Juventus mabao mawili hayo kipindi cha kwanza kabla ya Monaco kuamka na kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa Kylian Mbappe Lotin.
Juventus sasa inasubiri mshindi wa jumla kati ya Real Madrid na Atletico Madrid kwenye mechi ya nusu fainali ya pili mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Vicente Calderon.
No comments