FELLAINI AIPELEKA MAN UNITED FAINALI EUROPA LEAGUE

Manchester United imefanikiwa kutinga katika fainali ya michuano ya Europa league baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Celta Vigo kwenye mchezo wa marudiano wa nusu fainali katika dimba la Old Trafford.

Shujaa wa United usiku wa jana alikua ni Kiungo Maruane Fellaini ambaye alifunga kwa mpira wa kichwa baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Marcus Rashford kipindi cha kwanza.

Licha ya Celta Vigo kusawazisha bao hilo dakika ya 85 likifungwa na Facundo Roncaglia ambaye dakika 3 baadae kufuatia vurugu ambazo zilipelekea Eric Bailly wa Manchester United kutolewa pia kwa kadi nyekundu.

Kwa matokeo hayo Man United inafanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo kwa ushindi wa jumla wa bao 2-1 Baada ya matokeo ya ushindi wa bao 1-0 ugenini wiki iliyopita na fainali itakua tarehe 24 dhidi ya Ajax.

No comments

Powered by Blogger.