LICHA YA KUFUNGWA AJAX YATINGA FAINALI EUROPA LEAGUE


Fainali ya Michuano ya Europa League msimu huu itakua kati ya Ajax toka Uholanzi dhidi ya Manchester United ya England.

Ajax licha ya kutinga fainali imekumbana na kichapo cha bao 3-1 katika mechi ya marudiano ya nusu dhidi ya Olympic Lyon ya Ufaransa.

Faida ya ushindi walioupata wa bao 4-1 katika mechi ya awali ndiyo uliowaokoa wakifanikiwa kuvuka kwa ushindi wa jumla wa bao 5-4.

Fainali itapigwa wiki mbili zijazo katika mji mkuu wa Sweden.

No comments

Powered by Blogger.