ARSENAL YAIRUDISHA MAN UNITED NAFASI YA 6 LIGI KUU ENGLAND


Ushindi wa bao 2-0 walioupata Arsenal jana Usiku dhidi ya Southampton unawafanya sasa kufikisha pointi 66 na kupanda mpaka nafasi ya 5 huku wakiishusha Manchester United ambao walikua wakishikilia nafasi hiyo.

Iliwabidi Arsenal kusubiri mpaka kipindi cha pili kupata ushindi huo shukrani kwa magoli ya Alexis Sanchez na Oliver Giroud.

Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Arsenal baada ya mechi iliyopita kuwafunga Manchester United.

Vita ya kuwania kuwepo ndani ya timu nne za juu sasa inabaki kwa timu nne Liverpool,Manchester City,Arsenal na Man United huku Chelsea na Tottenham wakiwa tayari wameshajihakikishia na zikiwa zimebaki mechi 3 kwa kila timu.

No comments

Powered by Blogger.