SIMBA,KAGERA HAKUNA MBABE HUKUMU KUTOLEWA KESHO

Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF imeahirisha kutoa hukumu kuhusu timu ya Kagera Sugar kutoka kurejeshewa pointi tatu kufuatia kupinga hukumu iliyotolewa na Kamati ya masaa 72 iliyoipa Simba pointi tatu kwa kumchezesha Mohammed Fakhi mwenye kadi tatu za njano.

Kamati hiyo ambayo iliketi katika hotel ya Protea jijini Dar es Salaam imepitia Review hiyo na kuamua kuahirisha hadi kesho baada ya kutowahoji baadhi ya wahusika wa tukio hilo.

Katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa amewaambia waandishi wa Habari waliokuwepo hotelini hapo kuwa hukumu itatolewa kesho baada ya watu wote kuhojiwa ili Kamati itoe maamuzi ya haki.

"Ndugu zangu Waandishi wa Habari najua mmesubiri kwa muda mrefu ili kujua kilichoondelea kuhusu suala hili lakini tumeahirisha hadi kesho ili kuwahoji baadhi ya watu ambao kwa leo muda ilikuwa umeenda sana," alisema Mwesigwa

Wadau wa soka nchini walikuwa wakisubiri hukumu hiyo kwa hamu kutokana na kugusa hisia za timu kongwe za Simba na Yanga ambao ndiyo wanapigana vikumbo kutwaa taji hilo msimu huu.

No comments

Powered by Blogger.