LUDOVIC AACHIWA HURU SASA KUKIPIGA LYON MECHI ZILIZOBAKI

Mchezaji Ludovic Venance amefunguliwa kifungo chake baada ya ili kulinda kipaji chake kufuatia kusaini mkataba na African Lyon akiwa bado na mkataba na Mabao FC ya jijini Mwanza.


Maamuzi hayo yametolewa na Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF iliyoketi leo kupitia malalamiko mbalimbali na kutolea maamuzi suala hilo.

Ludovic amekosa mechi nyingi za msimu huu kutokana na sakata hilo lakini sasa anarejea ligi hiyo ikiwa inaelekea ukingoni huku timu yake ya Lyon ikiwa nafasi ya 11 kwenye msimamo.

Katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa alisema Kamati imechukuwa maamuzi hayo kwa kuangalia pande zote pomoja na kulinda kipaji cha mchezaji huku akiahidi kuchukuliwa hatua kiongozi wa Shirikisho hilo aliosababisha suala.

Wakati huo huo Mwesigwa alisema Lyon imepigwa faini ya shilingi laki tano baada ya kushindwa kufuatia kumsajili mchezaji huyo bila kufuata kanuni.

"Mchezo Ludovic Venance amefunguliwa na sasa atsichezea timu yake ya African Lyon lakini kiongozi aliyesababisha tatizo hili lazima nae achukuliwe hatua," alisema Mwesigwa.

No comments

Powered by Blogger.