SINGIDA UNITED YAPIGA HODI YANGA,AFRICAN LYON NA JKT RUVU LENGO NI KUPATA KIPA.
Katika kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya soka Tanzania bara klabu ya Singida United imeendelea kujiweka tayari na ligi hiyo na katika kutaka kuonyesha dhamira yao ya kufanya vyema msimu wao wa kwanza katika ligi klabu hiyo imeendelea kufanya usajili na safari hii wamegeukia upande wa kipa.
Timu hiyo yenye Makazi yake Mkoani Singida imeonyesha nia ya kumpata mmoja kati ya makipa watatu toka katika vilabu vya ligi kuu ambao ni Beno Kakolanya wa Yanga, Youthe Rostand raia wa Cameroon anayeichezea African Lyon na Said Kipao toka JKT Ruvu.
Mwishoni mwa wiki iliyopita Singida United ilikamilisha usajili wa nyota wawili wa Zimbabwe Elisha Moroiwa na Wisdom Mtasa wote toka Zimbabwe ikiwa tayari imeshamsajili awali mchezaji mwingine toka Zimbabwe lakini pia timu hiyo iko chini ya kocha Hans Van der Pluijm aliyekuwa kocha wa Yanga.

No comments