YANGA SASA KUCHEZA NA WAARABU CCM KIRUMBA MWANZA

Mabingwa wa Soka Tanzania bara na wawakilishi pekee waliobaki wa nchi katika michuano ya kimataifa Young Africans maarufu kama Yanga sasa watacheza mechi yao ya kwanza ya hatua ya mtoano katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Africa jijini Mwanza.


Habari ambazo www.wapendasoka.com imezipata na ambazo hazijawekwa wazi bado na wenyewe Yanga na hata shirikisho la Soka Nchini zimeeleza mechi hiyo ya awali ya hatua ya mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa katika ngazi ya klabu barani Afrika.

Yanga imepangwa kukutana na Wawakilishi wa Algeria MC Alger katika mechi ya awali tarehe 8/4/2017 kisha kurudiana wiki moja baadae huko Algeria.

Taarifa kuhusu mechi hiyo zimeeleza kwamba tayari mkaguzi wa Uwanja kutoka Shirikisho la Mpira wa miguu Barani Afrika CAF ambaye anatokea nchini Malawi ambaye yuko tayari jijini Mwanza na ameshafanya ukaguzi takribani 99% na ameridhika uwanja huo kutumika.

Kila la heri Yanga.

No comments

Powered by Blogger.