PIRLO: VERRATTI? HAPANA, HAKUNA MCHEZAJI ANAYECHEZA KAMA MIMI KWA SASA.


Kama uliwahi kufikiri kuwafananisha Marco Verratti na Andrea Pirlo basi badili fikra zako kwani Pirlo mwenyewe amesema kwa sana hakuna kiungo anayecheza kama yeye alnavyocheza mpira.

Andrea Pirlo anayekipiga huko Marekani katika timu ya New York City ameweka wazi kuwa kumekuwa na ukosefu wa kiungo mwenye uweza wa kuichezesha timu hasa katika miaka ya hivi karibuni. Anasema watu wanakosea sana kumfananisha na Marco Verratti wa PSG.


Akiongea na jarida la Corriere dello Sport Pirlo Amesema "watu wananifananisha mimi na Verratti, pamoja na kuwa namhusudu sana Verratti lakini watu watambue kuwa uchezaji wangu na wa Verratti uko tofauti sana. Namhusudu pia Roberto Gagliardini wa Inter lakini kila mmoja yuko na majukumu yake tofauti uwanjani"


Aliendelea Pirlo kwa kusema "Niwe muwazi tu, sioni kwa sasa mchezaji yeyote anayecheza vile mimi ninavyocheza, wapo viungo wengi sana wenye vipaji, lakini siyo viungo wa kariba yangu" Alimlizia Fundi huyo wa mpira.

Je, wewe unasemaje kuhusu maoni ya Pirlo, tuandikie hapo chini

1 comment:

  1. He is damn right! Pirlo alikua kwenye dunia ya akina Ronaldinho, Ronaldo "the Phenomenone" na Maradona. Wasimfananishe na vitu vya kijinga

    ReplyDelete

Powered by Blogger.