USHANGILIAJI ULIOACHA HISIA TOFAUTI KWA MASHABIKI


Kila mchezaji anapoingia uwanjani kucheza matarajio yake ni ushindi, lakini ushindi dhidi ya timu yako ya zamani huwa na hisia za kipekee kabisa. Kuifunga timu yako ya zamani siyo jambo la kushangaza kabisa lakini namna unavyoshangilia baada ya kuifunga tiu yako ya zamani ndiyo huwa kinaibua maswali mengi na hisia tofauti kwa wapenzi wa mpira wa miguu.

Wapo waliozifunga timu zao za zamani lakini waliishia kunyanyua mikono juu ishara ya kuomba msamaha, lakin wapo wengine waliofunga timu zao za zamani wakaishia kushangilia kana kwamba hawajawahi kuchezea timu hizo. Kushangilia huko mara nyingine kunakuwa ni kama kupigilia msumari wa moto kwenye vifua vya mashabiki wa timu iliyofungwa. Lakini pia wapo wachezaji wachache ambao mashabiki wanafurahia hata wakifungwa na wachezaji hao.

Tumekuwekea hapa wachezaji wachache waliowahi kushangilia baada ya kuzifunga timu zao za zamani. Wachezaji hao walishangilia kwa hisia na kupeleka ujumbe kwa mashabiki wakati mwingin kupelekea mashabiki kuwachukia wachezaji hao.

1.       Robin van Persie: Manchester United vs Arsenal
Baada ya kufunga magoli 132 katika misimu 8 aliyodumu Arsenal, Robin van Persie aliamua kutafuta maisha mapya ambayo yatampa furaha zaidi. Kocha wa Manchester United wakati huo Sir Alex Ferguson aliamua kumkaribisha Robin van Persie katika viunga vya Old Trafford kuja kujaribu bahati yake.


Robin alijaribu kuzuia hisia zake alipoifunga Arsenal katika dimba la Emirates, Lakini katika dimba la Old Trafford Robin alionyesha furaha ya aina yake mara baada ya kuifunga Arsenal akiunganisha kwa kichwa mpira uliopigwa na Wayne Rooney. Robin baada ya kufunga goli hilo alinyanyua mikono juu na kushangilia huku akimkimbilia Wayne Rooney ili wafurahie pamoja. Ilikuwa ni furaha ya aina yake lakini mwiba mkali sana kwa mashabiki wa Arsenal hasa baada ya kushuhudia mafanikio aliyoyapata Van Persie mara baada ya kuondoka Arsenal.

2.       Danny Welbeck: Arsenal vs Manchester United.
Amekuzwa na kufundishwa soka chini ya Manchester United, Usajili wake haukuwavutia mashabiki wengi wa Arsenal. Msimu wake wa kwanza kwa Arsenal haukuwa mzuri kutokana na kutawaliwa na majeruhi sana. Lakini aligeuka lulu hasa pale alipofunga goli muhimu lililopeleka Arsenal Nusu fainali na walifanikiwa kufika fainali na kuchukua kikombe cha Ligi (FA CUP) Msimu huo.



Welbeck atakumbukwa sana mara baada ya kuifunga timu yake iliyomlea na kumkuza Manchester United. Lakini nay eye welbeck hakuishia kufunga tu, bali alishangilia kuashiria kuwa yuko na furaha katika klabu ya mpya. Lilikuwa ni goli moja tu ambalo liliiondoa Manchester United katika mashindano hayo na furaha ya Welbeck ilikuwa juu zaidi hasa baada ya kuifunga Manchester United katika uwanja wao wa nyumbani Old Trafford.

3.       David Luis: PSG vs Chelsea
Hakujali misimu kadhaa aliyokaa Darajani kwa Chelsea, Hakujali Sura zilzile alizokuwa nazo bega kwa bega kupambana na miamba mingine ya ligi kuu England, kilichokuwa muhimu kwake ni Ushindi Klabu yake ya PSG. Huyo ndiye David Luis, Goli lake halitakuja kusahaulika kwani ni moja ya magoli yaliyozamisha meli yay a Chelsea na kushindwa kuvuka hatua ya 16 bora ya ligi ya klabu bingwa Ulaya.



Lakini hasira za mashabiki ziliisha na waliweza tena kumpokea kijana wa alipoamua kurudi nyumbani darajani mwaka 2016 akitokea katika klabu ya PSG kwa dau la £34m.

4.       Emmanuel Adebayor: Manchester City vs Arsenal
Katika msimu wa 2007/2008 Adebayor alifanikiwa kuifungia Arsenal magoli 30 katika mashindano yote, alikuwa mwiba kweli kwa timu pinzani. Lakini upendo wake ulitiliwa shaka alipokubali kuondoka London na kwenda kujiunga na Manchester City kwa dau la £25m.



Mashabiki wa Arsenal hawakufurahishwa na kitendo cha Adebayor kuhama kuondoka Arsenal, lakini Adebayor aliwakera zaidi baada ya kupiga usoni kipenzi chao Van Persie na alipelekea kufungia mechi tatu. Chakukumbwa zaidi katika mechi hiyo ni tukio alilolifanya Adebayor mara baada ya kuifunga Arsenal katika mechi hiyo.



Ulikuwa ni ushangiliaji wa aina yake na wenye hisia kali. Adebayor hakujali kuwa hawa walikuwa ndugu zake miezi kadhaa nyuma, hakujali namna walivyomshangilia wakati yupo nao, yeye alichojali muda ule ni kuonyesha hisia zake juu ya goli alilofunga. Mara baada ya goli hilo Adebayor alikimbia na kushangilia mbele ya mashabiki wa Arsenal na Alipoulizwa kwanini aliamua kushangilia vile, Adebayor alijibu ile ilikuwa ni kulipa kisasi kwa namna mashabiki wa Arsenal walivyokuwa wanadhihaki kwa kitendo chake cha kuhamia Manchester City.


Ni hayo tu kwa leo, je ni mchezaji gani unayemkumbuka ambaye naye aliwahi kushangilia mara baada ya kuifunga timu yake ya zamani.

Tuandikie maoni yako hapo chini kwenye kisanduku cha maoni.

No comments

Powered by Blogger.