MESSI AIBEBA BARCELONA KUIANGAMIZA ATLETICO MADRID KWAO
Goli la dakika ya 87 la mshambuliaji Lionel Messi lilitosha kuipa Barcelona ushindi muhimu ugenini wa bao 2-1 wakiifunga Atletico Madrid.
Mchezo huo uliotawaliwa kwa kiwango kikubwa na wenyeji Atletico Madrid ambao waliliandama vilivyo lango la Barcelona hasa kipindi cha kwanza lakini wakashindwa kabisa kupata bao.
Rafinha ndiye aliyefungua ukurasa wa mabao kwa Barcelona akifunga bao la kwanza dakika ya 64 kabla ya beki Diego Godin hajasawazisha dakika 6 badae lakini Messi akaja kuongeza bao la ushindi ambalo limeendelea kuweka matumaini kwa Barcelona kutetea ubingwa wao.

No comments