MOURINHO AANZA KUHESABU MAKOMBE MAN UNITED


Manchester United imekua timu ya kwanza msimu huu katika soka la England kushinda ubingwa msimu huu wakishinda ubingwa wa kombe la ligi nchini humo maarufu kama EFL.

Shujaa wa mchezo huo alikua Zlatan Ibrahimovic ambaye alifunga mabao mawili ya Man United katika ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Southampton.

Zlatan alitangulia kuifungia United bao la kwanza kwa njia ya mpira wa adhabu kisha Jesse Lingard akaongeza bao la pili kabla ya Manolo Gabbiadini hajasawazisha kwa upande wa Southampton akifunga mabao yote mawili kabla ya Zlatan hajafunga bao la tatu na la ushindi.

Jose Mourinho sasa anakua kocha wa kwanza kutwaa kombe hilo mara nyingi (mara nne) huku akiwa bado kocha huku Man United ikifikisha ubingwa wao wa tano katika historia.

No comments

Powered by Blogger.