MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUYAFAHAMU KUELEKEA MECHI YA FAINALI MAN UNITED VS SOUTHAMPTON LEO
Manchester United inatarajiwa kukutana na Southampton katika mechi ya fainali ya kombe la ligi nchini England (EFL) Kwenye dimba la Wembley jijini London kuanzia majira ya saa 1 usiku kwa saa za hapa Afrika Mashariki.
www.wapendasoka.com tumekuandalia baadhi ya mambo muhimu unayopaswa kuyajua kuelekea katika fainali hii
● Hii ni mara ya pili timu hizo zinakutana katika finali katika mashindano mara ya kwanza ikiwa fainali ya kombe la FA mwaka 1976 wakati Southampton waliposhinda bao 1-0 na kutwaa kombe hilo kombe ambalo ndiyo pekee ambalo Southampton wamebahatika kushinda katika historia yao.
● Southampton ni timu ya tatu ambayo inabahatika kucheza na Manchester United katika fainali ya kombe la FA na kombe la Ligi baada ya Aston Villa na Liverpool.
● Hii ni mara ya tisa Manchester United kucheza katika fainali ya kombe la ligi nchini England ikishinda kombe hilo mara 4 na kushindwa mara 4.
● Kocha Jose Mourinho ameweza kufika fainali za kombe hili la ligi mara tatu akiwa kama kocha wa Chelsea na kuahinda mara zote tatu yani 2005,2007 na 2015 akiwa ni kocha ws tatu mwenye mafanikio zaidi katika kombe hilo baada ya Brian Clough aliyeshinda mara 4 na Sir Alex Ferguson aliyeshinda mara nne pia.
● Zlatan Ibrahimovic amefunga magoli manne katika fainali 4 za kombe la ligi akiwa na Paris St-Germain.
● Southampton ni timu ya pili katika historia ya kombe la ligi nchini England kufika fainali bila kufungwa bao lolote timu ya kwanza kufanya hivyo ilikua Tottenham msimu wa wa 1981-82 lakini wakaja kupoteza kwa bao 3-1 kwenye fainali dhidi ya Liverpool.
● Kocha wa Southampton Claude Puel amefanikiwa kufika fainali ya michuano mikubwa mara moja tu mwaka 2001 wakati alipoifikisha Monaco katika fainali ya kombe la Ligi nchini Ufaransa wakipoteza kwa bao 2-1 toka kwa Lyon.

No comments